Waliongia robo fainali jana ndani ya Ngome Kongwe kwenye msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta Freestyle. Washiriki waliojitokeza walikuwa 24 na wamebaki wanane ambapo anatafutwa mkali mmoja tu. Mpambano unaendelea jioni hii.
Wakazi waMkongwe na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi jana kwenye msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta Style 2011.

Pichani mbele ni wasanii mahiri wa hip hop amba pia ni majaji wa shindano la Serengeti Freestyle 2011 wakifuatilia kwa makini. Kushoto ni Chiku Ketto kutoka kundi la The La Familia pamoja na Bonta kutoka The River Camp Soldier.

Wakali na mahiri wa kuangusha mangoma ndani ya Coconut FM, Boa pamoja na Yoram wakiendeleza kuwarusha washabiki waliofika kwenye mchanyato wa kuwasaka wakali wa Serengeti Fiesta Freestyle 2011.

No comments:
Post a Comment