Hatimaye zoezi lililochukua miezi kadhaa la kumtafuta mrembo mpya wa Tanzania kwa mwaka huu wa 2011(Miss Tanzania 2011),lilifikia kilele chake jana usiku katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam na mwanadada Salha Israel kuibuka mshindi na hivyo kuvikwa rasmi taji la Miss Tanzania 2011 kutoka kwa Genevive Emmanuel Mpangala(Miss Tanzania 2010) aliyekuwa akilishikilia taji hilo mpaka hapo jana.
Katika kilele cha shindano hilo lililodhaminiwa kwa kiasi kikubwa na kampuni ya Vodacom na kupambwa na burudani ya mziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wanaotamba Afrika Mashariki na Kati kama vile Diamond,Bob Junior,Kidumu na wengineo,mshindi wa pili alikuwa Tracy Sospeter na mshindi wa tatu akawa Alexia William.
Tunampongeza Salha kwa taji jipya.Lakini pongezi hizo ni vyema zikaenda na maswali magumu.Je,Salha anatoa matumaini kwa Tanzania kufanya Vizuri katika steji ya dunia(Miss World)?Je,Tanzania itaishia kuwa wasindikizaji tu katika fainali za dunia zinazotarajiwa kufanyika tarehe 6 November huko jijini London nchini Uingereza?Kuna lolote jipya ambalo Kamati Ya Miss Tanzania imejifunza kutokana na “uzoefu” wa miaka ya nyuma?
Upo ushauri ambao uliwahi kutolewa kwa kamati ya Miss Tanzania kupitia hapa BC.Je,umezingatiwa?Ni suala la kusubiri na kuona.
Miss Tanzania 2011,Salha Israel(katikati) akiwa na Tracy Sospeter(kulia-Mshindi wa Pili) na Alexia William(kushoto-Mshindi wa Tatu) mara baada ya kutangazwa mshindi.
No comments:
Post a Comment