MBUNGE wa Jimbo la Mvomero ,Amos Makalla,( CCM) ametoa vitabu 400 vyenye
thamani ya zaidi ya mamilioni ya shilingi vya mitaala ya masomo mbalimbali katika
Shule za Sekondari ya Kata ya Doma, ikiwa hatua ya kukabiliana na upungufu
wa vitabu na vifaa vingine kwenye shule za zilizojengwa kwa nguvu za
wananchi katika wilaya hiyo.
Vitabu hivyo vimekabidhiwa kwa ungozi wa Shule hiyo na Mbunge huyo wakati
wa mahafali ya pili ya kidato cha nne ya shule hiyo .
Mbunge huyo alikuwa mgeni rasmi , ambapo alitaja kuwa kati ya vitabu hivyo,
100 ni vya masomo ya sayansi yakiwemo ya fizikia,kemia ,bailojia na
hisabati.
Hata hivyo Mbunge huyo alisema, vitabu 300 ni masomo ya Jiografia,Hisabati
, lugha ya Kiswahili na kingereza na vitabu vya fasihi vya lugha hizo kuanzia
kidato cha kwanza hadi nne.
Mbali na kutoa vitabu hivyo, Mbunge huyo pia alitoa viti 50 kwa ajili ya
kukabilina na upungufu uliopo shuleni hapo kufuatia wanafunzi kukaa kiti na
meza moja zaidi ya mwanafunzi mmoja.
Hata hivyo Kabla ya kutoa misaada huyo, Mbunge huyo alishatoa mifuko 100 ya
saruji kwa ajili kukamilisha ujenzi wa madarasa ya shule hiyo , ambapo pia
ameahidi kuendelea kusaidia shughuli za maendeleo ya Kata hiyo.
Akizungumza na wahitimu watarajiwa wa kidato cha nne wa Shule hiyo ,
Makalla aliwataka wasibweteke na elimu ya kidato cha nne na badala yake
wajiendeleze hadi elimu ya juu ili kukabilina na changamoto mbalimbali za
ushindani wa soko la ajira.
Awali, Mkuu wa shule huyo,John Makarius,alisema wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo ya utoro ,mimba na wazazi kutokuwa na muamko wa
kugharamia watoto wao na kuwafanya wanafunzi 26 wakiume na wakike kati ya
72 kushindwa kuhitimu masomo yao.
Matatizo mengine ni pamoja na uhaba wa maji katika eneo hilo hali
inayopelekea kuchelewa kuanza kwa masomo kutokana na kutafuta maji kwajili
ya usafi wa mazingira ya shule.
Katika risala yao kuhitimu iliyosomwa na Abruhan Thabiti,aliomba uongozi wa
wilaya ya Mvomero kujenga kisima cha maji katika shule ili wanafunzi waweze
kuondokana na hadha kuchelewa masomo.
No comments:
Post a Comment