Monday, September 19, 2011

MIMS IN AN EXCLUSIVE COLLABO AT BONGO RECORDS

Siku chache zijazo,studio inayomilikiwa na P-Funk aka Majani ya Bongo Records itakuwa inapaa katika anga za kimataifa pale itakapoachia kitu ambacho kimemshirikisha msanii maarufu kutoka nchini Marekani anayekwenda kwa jina la MIMS(pichani).

Kwa mujibu wa habari ambazo BC imezipata,msanii MIMS ambaye ana asili ya Jamaica na mkazi wa maeneo ya Washington Heights huko New York, atashirikiana na wasanii kadhaa wa Tanzania katika track hiyo.Orodha kamili ya wasanii ambao watashirikishwa katika kibao tarajiwa bado haijawekwa wazi lakini tetesi zinapasha kwamba watakuwa ni wasanii wakali kutoka Bongo.

Miongoni mwa nyimbo za MIMS ambazo ziliwahi kufanya vizuri sana katika chati za muziki ulimwenguni ni pamoja na ule wa This Is Why I am Hot. Siku chache zijazo,studio inayomilikiwa na P-Funk aka Majani ya Bongo Records itakuwa inapaa katika anga za kimataifa pale itakapoachia kitu ambacho kimemshirikisha msanii maarufu kutoka nchini Marekani anayekwenda kwa jina la MIMS(pichani).

Kwa mujibu wa habari ambazo BC imezipata,msanii MIMS ambaye ana asili ya Jamaica na mkazi wa maeneo ya Washington Heights huko New York, atashirikiana na wasanii kadhaa wa Tanzania katika track hiyo.Orodha kamili ya wasanii ambao watashirikishwa katika kibao tarajiwa bado haijawekwa wazi lakini tetesi zinapasha kwamba watakuwa ni wasanii wakali kutoka Bongo.

Miongoni mwa nyimbo za MIMS ambazo ziliwahi kufanya vizuri sana katika chati za muziki ulimwenguni ni pamoja na ule wa This Is Why I am Hot.

No comments: