Monday, October 10, 2011

DR.MWAKYEMBE ANAUGUA:TUNAMTAKIA HERI APONE

Afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi,Dr.Harrison Mwakyembe sio njema.Hiyo ni kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari likiwemo  Gazeti la Mwananchi, Dr Mwakyembe anaugua ugonjwa wa ngozi ambao kwa kitaalamu unajulikana kama Exfoliative Dermatitis ambao pamoja na karaha zingine husababisha kuwashwa,kuishia nguvu na sehemu ya juu ya ngozi kupukutika.
Pizaz5 inaungana na wote katika kumtakia heri Dr.Harrison Mwakyembe apone haraka ili hatimaye aweze kurejea katika majukumu yake ya kawaida.
Pichani juu ni Dr.Harrison Mwakyembe akiongea na Rais Jakaya Kikwete pale Rais Kikwete alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake maeneo ya Kunduchi Beach(Mtongani) katika viunga vya jiji la Dar-es-salaam.

No comments: