Thursday, October 27, 2011

MISS WORLD 2011:NINI MATUMAINI YA TANZANIA?

Pichani ni Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Israel,akipunga mkono wa kwaheri kwa baadhi ya ndugu,jamaa,marafiki na watanzania waliojitokeza kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere(JNIA) jijini Dar-es-salaam hapo jana.
Salha ameondoka kwenda kushiriki katika mashindano ya dunia (Miss World) yatakayofanyikia jijini London nchini Uingereza mwezi ujao tarehe 6 Novemba katika ukumbi wa Earls Court Two ambapo mshindi wa Miss World 2010,Mmarekani Alexandria Mills atakabidhi taji lake kwa mshindi mpya.
Swali kubwa ambalo najiuliza na ningependa nawe msomaji ujiulize ni kwamba je,mwaka huu Tanzania ina matumaini ya kufanya vizuri zaidi kuliko miaka ya nyuma?Tumefanya maandalizi ya kutosha ili kwenda kushindana na sio kushiriki katika mashindano haya?Na endapo tutaishia kuwa wasindikizaji,mwakani tujiandae namna gani?Tuwapate vipi wanaokwenda kutuwakilisha?
Bila shaka majibu ya baadhi ya maswali hayo magumu yapo mikononi mwa Kamati ya Miss Tanzania.

No comments: