Wednesday, May 4, 2011
LULU ACHUMBIWA
Zikiwa zimekatika wiki mbili tangu alipoangusha bonge la ‘pati’ kusherehekea kutimiza miaka 18, nyota kinda wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amechumbiwa, Ijumaa lina ‘eksiklusivu’.
Akizungumza na gazeti bora la burudani Bongo, Ijumaa jijini Dar es Salaam juzi, Lulu alifunguka kwamba, kwa muda mrefu amekuwa akikutana na usumbufu wa midume ikimtaka kimapenzi na maneno pekee kuwa ana mchumba yalikuwa hayawaingii kichwani.
Alisema kuwa, kwa kumheshimu mchumba wake wa siku nyingi, ameamua kutupia pete hiyo katika kidole chake cha pete ‘chanda’ ili kuondokana na usumbufu huo.
Msanii huyo asiyeishiwa matukio alitambaa na mistari kuwa, pete hiyo ni ushahidi kwamba kwa sasa amechumbiwa na mwanaume aliyemtaja kwa jina moja la Denis aishie nchini Sweden.
Alisema: “Msishangae sana jamani, hii pete ni ishara kuwa nimechumbiwa.
“Msitake kumjua zaidi mume wangu mtarajiwa ila ni Mtanzania ambaye kwa sasa yuko Sweden kikazi, naomba ieleweke hivyo na sitaki mapaparazi wamchimbe ndiyo maana nimewatajia jina moja.
“Ukweli ni kwamba tangu siku nyingi alikuwa akinisubiri nitimize miaka 18 ili asikumbane na mkono wa sheria. Nawahakikishia yuko mbali na mimi kwa sasa lakini ananijali na kunisaidia katika maisha yangu ya kila siku.
“Nina imani sasa nitakuwa huru na wanaume wataacha kunisumbua wakijua kuwa nina mwanaume wangu ninayempenda kupita maelezo.”
Aidha, baadhi ya watu waliozipata habari za Lulu kuvishwa pete walishangaa na kuhoji kama kwa jinsi wanavyomfahamu ataimudu mikiki ya ndoa.
Juhudi za kumpata mama wa Lulu ili kuthibitisha tukio la mwanaye kuchumbiwa ziligonga mwamba baada ya simu yake kutokuwa hewani kila ilipopigwa.

Labels:
news
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment