Thursday, March 29, 2012

TETESI: Ukosefu wa fedha, Tanzania hatarini kuanza mgao wa umeme.

Makao Makuu ya Tanesco, Jijini Dar Es Salaam.
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imetahadharisha kuwa kuna uwezekano kwaTanzaniakuingia kwenye mgao mwingine wa umeme kutokana na ukosefu wa fedha za kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura.
Tahadhari hiyo imetolewa wakati ambapo Serikali imepanga kulidhamini Shirika la Umeme nchini, TANESCO, ili liweze kukopa shilingi Billion 408 kwa ajili ya kujiendesha kutokana na ukame wa mara kwa mara.
Ingawa shirikahilolinahitaji shilingi bilioni 408 za mkopo ili kununua mafuta ya kuendeshea mitambo yake lakini bado linadaiwa shilingi bilion 269 na baadhi ya kampuni za kuzalisha umeme na hivyo kuonekana kuwa bado ni kiasi kidogo kutokana na fedha zote zitakazopatikana zinategemewa kupelekwa katika ulipaji wa madeni hayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Mheshimiwa January Makamba anasema hadi sasa hakuna fedha za kuendeshea mitambo na tayari kampuni mbalimbali za kuzalisha umeme zimezima mitamboyaokutokana na kuidai TANESCO kiasi kikubwa cha fedha.
Hadi sasa kampuni ya kuzalisha umeme ya Agreko imezima mitambo yake iliyokuwa inaingiza kwenye Gridi ya Taifa Megawati 100 kutokana na kuidai TANESCO zaidi ya shilingi bilioni 230 na hivyo kupunguza idadi za Megawati kwenye Gridi ya Taifa kutoka 600 na kufikia 500 kwa hivi sasa.
Hata hivyo bado mfumo wa kusafirisha pamoja na kusambaza umeme haipo katika imara unaotakiwa katika kipindi cha muda mrefu ingawa Mheshimiwa Makamba anashauri kuwa ukombozi wa matatizo yaliyopo katika uzalishaji wa nishati hiyo yatakwisha endapo matumizi ya nishati ya gesi yatapewa nafasi badala ya mafuta.
Taarifa hiyo ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini inaweza kusababisha hofu kwa wananchi ambao bado hawajamaliza machungu waliyonayo kutokana na kipindi kirefu cha mgao uliomalizika miezi michache iliyopita.

No comments: