Thursday, March 29, 2012

Mali:Amadou Toumani Toure asema yuko huru na salama.

Raisi wa Mali aliyepinduliwa Amadou Toumani Toure
Raisi wa Mali aliyepinduliwa Amadou Toumani Toure akikagua Majeshi siku chache kabla ya kupinduliwa.
Raisi wa Mali aliyepinduliwa , japo hajulikani yuko wapi , amenukuliwa akisema yuko huru na salama kabisa. Toure amekanusha habari kuwa anashikiliwa na wanajeshi ambao siku ya tarehe 22 walipindua serikali yake. Na maelfu wa raia wa Mali walionekana kuijibi jumuiya ya Afrika mangharibi ECOWAS kwa kujitokeza barabarani na kufanya maandamano yakuunga mkono mapindizi ya kijeshi.
Awali ECOWAS ilitoa onyo kali kwa viongozi wa kijeshi waliopindua serikali ya Rais Amadou Toumani Toure na kuwataka wayakabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.
Nao waandamanaji wanadai kuwa ECOWAS haijui tabu waliokuwa wanapata chini ya utawala wa Toure. Kupinduliwa kwa Rais huyo wa Mali kulitokea kukiwa kumesalia wiki tano peke yake ili uchaguzi mkuu ufanywe.
Lakini mara tu baada ya kumtimua madarakana bwana Toure, baraza la jeshi linaloongoza nchi lilitangaza kuhairishwa kwa uchaguzi huo kwa muda usiojulikana. Katika taarifa yake fupi kwa njia ya simu kwa shirika la habari la AFP alisema lilio muhimu kwa wakati huu ni kufahamisha watu kuwa yuko huru wala hazuiliwa kama inavyodaiwa.
“Nafuatilia kwa makini sana yale yote yanayotokea nchini. Kwa moyo wangu wote nataka amani na demokrasia”, Toure alisema.
Kwa siku sita mfululizo kumekuwa na taarifa za kutatanisha kuhusu mahali alipo Raisi huyo mwenye umri wa miaka 63.

No comments: