Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015 na kutamba kuwa ana nafasi nzuri kutokana na sifa alizojijengea ndani ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Sitta alitaja sifa hizo kuwa ni pamoja ile ya kuwa mteule wa rais, kwa awamu zote nne za uongozi taifa, tangu Tanzania ilipotaka uhuru wake, Desemba 9 1961.
Spika huyo mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , alisema kwa sasa anawasikiliza wananchi kama wataona anafaa na haoni ubaya wowote wa kushika nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa taifa kwa miaka mitano tu na kuwaachia vijana waendelee.
Alisema kuwa ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2014, kila kitu kitakuwa wazi na hawezi kukataa majukumu atayopewa na wananchi wake kwani anatambua wanamuamini kwamba ana uwezo wa kuchapa kazi.
Sitta ambaye pia ni Mbunge Urambo Mashariki na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa( NEC) ya CCM, aliyasema hayo jana muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani kufunga kampeni za udiwani za CCM, Kata ya Kirumba.
No comments:
Post a Comment