Monday, April 2, 2012

LIVE BILA CHENGA !! CHADEMA YASHINDA UCHAGUZI ARUMERU

Mbunge wa Arumeru Mashariki Ndugu Joshua Nassari
“Ninawashukuru sana watu wa Arumeru Mashariki ambao hawakujali umri wangu, uwezo wangu kifedha, historia ya familia yangu katika siasa, na mapungufu niliyokuwa nayo lakini wakakubali kunichagua!
Najua walikuja wengi na fedha nyingi,
Najua walikuja wengi na majina makubwa,
Najua walikuja wengi na kila aina ya mbwembwe,
Najua walikuja wengi na bendi nyingi na wakahonga sana,
Najua walikuja wengi wakanitukana na kunisema sana! Lakini hatimaye sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, na lile alilolipanga mwenyezi Mungu limekwenda kutimilika!

Walipoambiwa mimi ni mdogo kiumri, walisema siendi bungeni kupeleka mvi au miaka, na wakasema wanahitaji dogo janga na si kubwa jinga,
Walipoambiwa mimi sijaoa, wakasema mimi siendi bungeni kusuluhisha ndoa,
Walipoambiwa mimi ni masikini, walisema wanahitaji masikini mwenzao,
Walipoambiwa sina kitambi, walisema bungeni siendi kucheza mieleka…” MBUNGE MTEULE, ARUMERU MASHARIKI, JOSHUA NASSARI, BAADA YA USHINDI!


Hati ya Ushindi ya Kuchaguliwa kuwa Mbunge aliyokabidhiwa Ndugu Joshua Nassari
Mbunge Mteule Nassari  - Kura 32,972
 Bw. Sioi Sumari - Kura 26,757
Vyama vingine : DP - Kura 77
                           NRA - Kura 35
                           AFP - Kura 139
                           UPDB - Kura 18
                           TLP - Kura 18
                           SAU - Kura 22

Sunday, April 1, 2012

SAMUEL SITTA AKUBALI KUUTAKA URAIS 2015

Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015 na kutamba kuwa ana nafasi nzuri kutokana na sifa alizojijengea ndani ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Sitta alitaja sifa hizo kuwa ni pamoja ile ya kuwa mteule wa rais, kwa awamu zote nne za uongozi taifa, tangu Tanzania ilipotaka uhuru wake, Desemba 9 1961.
Spika huyo mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , alisema kwa sasa anawasikiliza wananchi kama wataona anafaa na haoni ubaya wowote wa kushika nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa taifa kwa miaka mitano tu na kuwaachia vijana waendelee.
Alisema kuwa ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2014, kila kitu kitakuwa wazi na hawezi kukataa majukumu atayopewa na wananchi wake kwani anatambua wanamuamini kwamba ana uwezo wa kuchapa kazi.
Sitta ambaye pia ni Mbunge Urambo Mashariki na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa( NEC) ya CCM, aliyasema hayo jana muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani kufunga kampeni za udiwani za CCM, Kata ya Kirumba.

Thursday, March 29, 2012

Mali:Amadou Toumani Toure asema yuko huru na salama.

Raisi wa Mali aliyepinduliwa Amadou Toumani Toure
Raisi wa Mali aliyepinduliwa Amadou Toumani Toure akikagua Majeshi siku chache kabla ya kupinduliwa.
Raisi wa Mali aliyepinduliwa , japo hajulikani yuko wapi , amenukuliwa akisema yuko huru na salama kabisa. Toure amekanusha habari kuwa anashikiliwa na wanajeshi ambao siku ya tarehe 22 walipindua serikali yake. Na maelfu wa raia wa Mali walionekana kuijibi jumuiya ya Afrika mangharibi ECOWAS kwa kujitokeza barabarani na kufanya maandamano yakuunga mkono mapindizi ya kijeshi.
Awali ECOWAS ilitoa onyo kali kwa viongozi wa kijeshi waliopindua serikali ya Rais Amadou Toumani Toure na kuwataka wayakabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.
Nao waandamanaji wanadai kuwa ECOWAS haijui tabu waliokuwa wanapata chini ya utawala wa Toure. Kupinduliwa kwa Rais huyo wa Mali kulitokea kukiwa kumesalia wiki tano peke yake ili uchaguzi mkuu ufanywe.
Lakini mara tu baada ya kumtimua madarakana bwana Toure, baraza la jeshi linaloongoza nchi lilitangaza kuhairishwa kwa uchaguzi huo kwa muda usiojulikana. Katika taarifa yake fupi kwa njia ya simu kwa shirika la habari la AFP alisema lilio muhimu kwa wakati huu ni kufahamisha watu kuwa yuko huru wala hazuiliwa kama inavyodaiwa.
“Nafuatilia kwa makini sana yale yote yanayotokea nchini. Kwa moyo wangu wote nataka amani na demokrasia”, Toure alisema.
Kwa siku sita mfululizo kumekuwa na taarifa za kutatanisha kuhusu mahali alipo Raisi huyo mwenye umri wa miaka 63.

TETESI: Ukosefu wa fedha, Tanzania hatarini kuanza mgao wa umeme.

Makao Makuu ya Tanesco, Jijini Dar Es Salaam.
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imetahadharisha kuwa kuna uwezekano kwaTanzaniakuingia kwenye mgao mwingine wa umeme kutokana na ukosefu wa fedha za kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura.
Tahadhari hiyo imetolewa wakati ambapo Serikali imepanga kulidhamini Shirika la Umeme nchini, TANESCO, ili liweze kukopa shilingi Billion 408 kwa ajili ya kujiendesha kutokana na ukame wa mara kwa mara.
Ingawa shirikahilolinahitaji shilingi bilioni 408 za mkopo ili kununua mafuta ya kuendeshea mitambo yake lakini bado linadaiwa shilingi bilion 269 na baadhi ya kampuni za kuzalisha umeme na hivyo kuonekana kuwa bado ni kiasi kidogo kutokana na fedha zote zitakazopatikana zinategemewa kupelekwa katika ulipaji wa madeni hayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Mheshimiwa January Makamba anasema hadi sasa hakuna fedha za kuendeshea mitambo na tayari kampuni mbalimbali za kuzalisha umeme zimezima mitamboyaokutokana na kuidai TANESCO kiasi kikubwa cha fedha.
Hadi sasa kampuni ya kuzalisha umeme ya Agreko imezima mitambo yake iliyokuwa inaingiza kwenye Gridi ya Taifa Megawati 100 kutokana na kuidai TANESCO zaidi ya shilingi bilioni 230 na hivyo kupunguza idadi za Megawati kwenye Gridi ya Taifa kutoka 600 na kufikia 500 kwa hivi sasa.
Hata hivyo bado mfumo wa kusafirisha pamoja na kusambaza umeme haipo katika imara unaotakiwa katika kipindi cha muda mrefu ingawa Mheshimiwa Makamba anashauri kuwa ukombozi wa matatizo yaliyopo katika uzalishaji wa nishati hiyo yatakwisha endapo matumizi ya nishati ya gesi yatapewa nafasi badala ya mafuta.
Taarifa hiyo ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini inaweza kusababisha hofu kwa wananchi ambao bado hawajamaliza machungu waliyonayo kutokana na kipindi kirefu cha mgao uliomalizika miezi michache iliyopita.

Royal bakery iliyopo kawe yavamiwa na majambazi usiku huu,wakomba fedha za mauzo na kuwalaza chini wafanyakazi


Baadhi ya wafanayakazi wa Bakery wakiwa wanashangaa punde tu baada ya kuvamiwa na
Majambazi waliopora fedha za mauzo.

Masikini Dada wa watu akilia kwa uchungu,huku polisi wakiendelea kuchukua maelezo.

DALADALA ZAGOMA JIJINI MWANZA


wakazi wa jiji la Mwanza wakiwa wamepanda gari la mizigo imebeba abiria kuelekea mjini.

Baada ya Madereva wa usafiri wa daladala katika barabara iendayo Kilimahewa jijini mwanza kuweka mgomo baridi, halmashauli ya jiji la mwaza imeanza ukarabati wa barabara katika kiwango cha changarawe..  
Hatua hiyo imekuja kufuatia kuharibika kwa barabara hiyo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini mwanza na hivyo kuhofia  kuharibu magari na kusababisha ajali zisizo za lazima.
Barabara hii ambayo hutumiwa na wakazi toka katika vitongoji vitano vikiwemo kilimahewa, nyasaka, Kiloleli,Maduka tisa na kaburi moja imekuwa mbovu kwa kipindi kirefu.
Jambo hili lilipelekea madereva wa daladala wanao fanya safari zao katika eneo hili kufanya mgomo baridi mapema leo asubuhi na hii kuathiri shughuli za wakazi wa eneo hili katika swala zima la usafiri.  
Mapema asubuhi wanachi walionekea wakitembea kwa wamiguu kuelekea katika shughuli zao huku waendesha pikipiki maarufukamaboda boda kuchukua abiria hao kwa gharama ya shilingi 2000 na kuendelea.
Wananchi walionyesha  hasira zao kwa viongozi waliowachagua na kutupa lawama kwa halmashauri ya jiji la mwanza kutokana na tatizohilola barabara hiyo kuwa sugu.
Madereva wa daladala katika barabara hiyo walionyesha  dhamira yao ya kutoendelea kutoa huduma hiyo hatakamabarabara hiyo haitakarabatiwa kwa kipindi kirefu.
Mwenyekiti wa umoja cha madereva wa daladala kanda ya ziwa Dede…alimesema maamuzi hayo yamefikiwa kufuatia kupuuziwa kwa baruayaoyaliyoiandikia halmashauri ya jiji juu ya ubovu huo wa barabara.
Malalamiko hayo na ubovu wa barabara ya kilimahewa inatusukuma mpaka katika ofisi za halmashauri ya jiji la mwanza ambapo kaimu mkuurugenzi Jeremiah Tito anakiri ubovu wa barabara hiyo.
Alifafanua kuwa halmashauri ya jiji imetenga bajeti ya dharura shilingi milioni 200 kushughulikia miundombinu iliyoharibiwa na mvua zilizonyesha novemba 14 na kusababisha mafuriko.
Mpaka taarifa hii inakwenda hewani tayari barabara hii ilikuwa imeanza kufanyiwa ukarabati kwa zaidi ya kilomita moja,juhudi zetu zakuwapa uongozi wa madereva kufahamukamamgomo huu utenedelea hazikufua dafu.
  Wamiliki wa Dalada wakiwa wamepaki vyombo vyao vya usafiri mbele ya ofisi za wilaya
 Mwenyekiti wa chama cha madereva wa daladala kanda ya ziwa Protas Dede amewaomba radhi wananchi kwa hali iliyotokeza na usumbufu walioupata kwani imewabidi kutetea haki ili mambo yaende sawa

CCM NA CHADEMA ... Waonesha Makucha Arumeru

Mh. Livingstone Lusinde akimwaga Sera za CCM Arumeru


Thursday, March 22, 2012

KAMPENI ZA ARUSHA, CCM YAZIDI KUNADIWA

Kina mama wakimbeba Sioi baada ya kuhutubia mkutano wa kapeni kijiji cha Mulala kata ya Songoro Jimbo la Arumeru Mashariki.   


Mjumbe wa NEC Oganaizesheni CCM, Asha Abdallah Juma akihutubia mkutano wa kampeni kijiji cha Sura

Monday, March 19, 2012

Wapinzani wa ligi Kuu bara

Kikosi cha Yanga 
Kikosi cha Simba

Lowassa awakaanga vigogo Serikali ya JK

                                                               Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa 

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema anashangazwa na Serikali kuendelea kulifumbia macho tatizo la ajira kwa vijana na kuwaomba maaskofu wasaidie kulimaliza akisema hilo ni bomu linalosubiri kulipuka.
Lowassa alisema hayo jana alipokuwa akitoa salamu zake kwenye sherehe za uzinduzi wa jimbo jipya la Kanisa Katoliki la Ifakara zilizofanyika katika Viwanja vya Kanisa Kuu la Mtakatifu Edward, Ifakara.
Alisema viongozi wa juu serikalini wameshindwa kulitatua na kulifumbia macho tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana hivyo kuwaomba maaskofu waliangalie kundi hilo ambalo linakabiliwa na changamoto nyingi.
“Suala la ajira kwa vijana hakuna kiongozi anayelishughulikia ipasavyo ndani ya Serikali, hivyo niwaombe maaskofu nchini walione hili. Nawaomba katika miradi yenu mlipe kipaumbele suala la tatizo la ajira kwa vijana,” alisema Lowassa na kuongeza:
“Kanisa Katoliki limekuwa likisaidia sana katika sekta ya elimu na afya kwa hiyo sasa waelekeze nguvu hizo katika kusaidia ajira kwa vijana. Wengi wanaomaliza elimu ya sekondari na vyuo wanakabiliwa na tatizo kubwa la ajira. Hili kama tunavyosema ni bomu linalosubiri kulipuka, sasa naliomba Kanisa lisaidie juhudi za Serikali kutatua tatizo hili,” alisema Lowassa huku akishangiliwa.

Ruwaichi na mgomo
Akizungumza katika sherehe hizo, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Yuda Dadeus Ruwaichi alisema mgomo wa madaktari nchini umedhihirisha udhaifu wa Serikali katika kushughulikia migogoro na kusema ni aibu kwa Tanzania.
“Watu wengi wamekufa katika mgomo ule na hii imeonyesha Tanzania ni taifa lisilo na dira,” alisema Askofu Ruwaichi huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda ambaye ni Mbunge wa Ulanga Mashariki akimsikiliza.
“Hakuna hata uharaka uliochukuliwa kushughulikia mgomo ule na hii ni kwamba nchi yetu sasa imefikia pabaya kwani inaonekana imeshindwa kushughulikia matatizo,” alisisitiza.
Katika salamu hizo kwa Askofu mpya wa jimbo jipya la Ifakara, Salutaris Libena, Askofu Ruwaichi alisema kanisa litaendelea kupiga vita umasikini.

Alimtaka askofu huyo kutoogopa kukemea maovu yanayofanywa na viongozi wa Serikali na kusababisha pengo kati ya wenye nacho na wasionacho.

Mwinyi asisitiza upendo
Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi alimtaka Askofu Libena kutumia nafasi yake kuleta amani na upendo miongoni mwa waumini wa dini mbalimbali.

Mwinyi alisema uaskofu ni daraja kubwa linalofanana na nafasi ya uwaziri katika Serikali hivyo waumini wa dini ya Kikristo katika jimbo jipya la Ifakara wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kiongozi huyo aliyesimikwa kutumikia dini hiyo na Watanzania kwa ujumla.

“Nafasi ya uaskofu haifungamani na dini wala kabila kwani daraja hilo limejaa roho ya huruma na upendo hivyo jamii ya jimbo la Ifakara ni wakati wa kutoa ushirikiano ili kumpa nafasi mhashamu Askofu Salutari Libena ya kuwahudumia katika nyanja mbalimbali za elimu, afya na tabia njema,” alisema Mwinyi.

Kadinali Pengo
Katika mahubiri yake, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo alisema uamuzi wa kugawanya Jimbo la Mahenge ni mchakato wa muda mrefu uliotokana na ukubwa wa Jimbo la Mahenge.

“Mchakato huo uliridhiwa na Papa Benedict wa 16 Januari 14, 2012 kwa kukubali Ifakara kuwa jimbo jipya na makao makuu katika Kanisa la St Andrew lililopo mji mdogo wa Ifakara.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini na taasisi wakiwemo maaskofu wa majimbo 34.

Wengine waliohudhuria sherehe hizo ni Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga na Kilombero, Francis Miti. 

MWAKYEMBE: Mjadala wa AFYA yangu UMEFUNGWA! ! !

Hapa mwakyembe akiwasili kwa nguvu zote




Hapo mwakyembe akielekea ofisini


Mwakyembe akiongea na waandishi wa Habari na kunena kuwa mjadala
umefungwa full stop hakuna mtu kujadili tena afya yake inaendelea vizuri


Muamba bado mahtuti , Abidal nae wengi wazidi kumuombea

Wachezaji wa Real Madrid ya Hispania wakionesha kumtakia hali njema mchezaji Abidal wa Ufaransa na Barcelona.
Mashabiki wa Mpira wa Miguu ligi ya uingereza wakionesha kujali na kumuombea mchezaji wa Bolton 
Fabrice Muamba apate nafuu haraka.

BINTI WA WHITNEY AKATA MZIZI WA FITINA...

Ama kweli mtoto huyu 'amepinda." Bobbi Kristina akitoka kwenye duka la AT&T huku akianika pete yake ya uchumba. Kulia akiwa ameambatana na mchumba wake, Nick Gordon. 

Katibu Mkuu Ofisi Ya Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar Azindua Ripoti ya Utafiti wa Hali ya Utendaji Wa Vyombo vya Utangazaji vya Umma Zanzibar

KATIBU Mkuu ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais, Dk. Omar Dadi Shajak akionesha ripoti ya utafiti wa hali ya utendaji wa Vyombo vya Utangazaji vya Umma Zanzibar muda mfupi baada ya kuizindua ripoti hiyo katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani,kulia Meneja wa Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar, Suleiman Seif 
KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais, Dk. Omar Dadi Shajak akizinduwa Ripoti ya Utafiti wa Hali ya Utendaji wa Vyombo vya Utangazaji vya Umma Zanzibar, uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani.Picha na Haroub Hussein 

MATOKEO YA MECHI ZA JUMAPILI, PREMIER LEAGUE, FA CUP, PRIMERA DIVISION NA BUNDESLIGA

Manchester United's Antonio Valencia drives in their second goal at Molineux on Sunday 

Maiti azua mtafaruku

MTAFARUKU mkubwa umeibuka wa kugombea maiti na mali zake, kati ya ndugu wa  marehemu, mumewe na mwajiri. Dada wa marehemu anadai kadi za benki huku mwajiri naye akitaka vyombo vya ndani kwa madai kuwa fedha alizovinunulia alikopa kazini.  Rahima Hamad (24) alifariki dunia Machi 4 katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, mkoani Kilimanjaro baada ya kujifungua mtoto njiti, hospitalini hapo.  Akizungumza na gazeti hili jana, mume wa marehemu, Matheo Juma, alidai kuwa yeye na mkewe (marehemu), waliishi kwa miaka sita, lakini cha kusikitisha ni kwamba upande wa familia ya marehemu wamekana kumtambua.  Alidai kwamba awali ndugu wa mkewe walikuwa wakifika nyumbani kwake na kupata huduma mbalimbali, lakini baada ya kifo hicho wamemkana na kudai kuwa marehemu hakuwa na mume, hivyo mazishi hayawezi kufanyika sehemu nyingine tofauti na alikozaliwa kijijini kwao Rombo.  Juma alidai kuwa awali mkewe alikuwa Mkristo, na kubadilisha dini kwa ridhaa yake kuwa Mwislamu, na kisha kutambulishwa kwa wazazi wa mke kwa ajili ya mchakato wa kufunga ndoa naye.  Alisema mara baada ya msiba huo kutokea kaka wa marehemu, Doe Swai, alimkana na akidai kuwa dada yao hakuwa na mume, huku akimtuhumu yeye kuhusika na kifo hicho kutokana na ujauzito, hivyo maiti lazima azikwe kwa misingi ya kikristo.  Juma aliendelea kudai kwamba mbali na hilo, pia dada wa marehemu aliyetambuliwa kwa jina la Eliza na mwajiri wa marehemu, Stella Sembeti, wanadai mali zilizoachwa na marehemu vikiwamo vyombo vya ndani, kadi za benki na nguo wakati huu ambao hata maziko hayajafanyika.  Alidai kwamba kutokana na hali hiyo, ametishiwa maisha endapo atahudhuria  mazishi na kama ataendelea kung’ang’ania mwili wa marehemu.  Kwa upande wao, majirani wa marehemu walisema wakati mwajiri na dada wa marehemu walipofika kudai mali hizo, wananchi walijikusanya kwa lengo la kuwapiga lakini fujo hizo zilitulizwa na Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa na kuamuru vyombo hivyo vihamishwe ili viwekwe sehemu yenye usalama kwa usimamizi wake.  Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Eliza alikiri kuwapo mvutano huo, na kueleza kuwa hawezi kumtambua mwanamume aliyekuwa akiishi na dadake kwani hana cheti cha ndoa, na mila za Wachaga haziruhusu azikwe nje ya familia.  Eliza alisema uamuzi wa kumzika marehemu nyumbani kwa wazazi wake unazingatia wosia alioandika marehemu na kuwaeleza watoto wake kuwa akifariki dunia azikwe kwa baba na mama yake.  Alisema mbali na hayo, hawezi kumtambua kwa sababu hajawahi kutoa mahari, hivyo hana uhalali na mwili wa marehemu, huku akidai kuwa mali zote ni za marehemu kwa kuwa mume huyo hakuwa na kitu chochote tangu walipoanza kuishi.  Eliza alieleza kuwa mdogo wake awali aliolewa na mume mwingine kwa ndoa ya Kanisa Katoliki, hivyo anayedai kuwa mumewe wa sasa alimnyang’anya mume mwingine, hivyo akahamishia mali zote kwake.  Akizungumzia mali anazozidai, Eliza alisema mali zote ni za dada yao, na kuwa kadi ya benki marehemu aliihamishia kusikojulikana; na wakati mazungumzo na gazeti hili yakiendelea Eliza alinyang’anywa simu na mwanamume ambaye alidai, “hapa tupo kwenye msiba,” na kukata simu na kuizima.  Gazeti hili pia lilimpata aliyekuwa mwajiri wa marehemu –Sembeti, ambaye alikiri Rahima (marehemu) alikuwa mfanyakazi wake katika hoteli ya Kiusa Pub akiwa Meneja mjini hapa. Akizungumzia madai ya kutaka mali za ndani za Rahima, alisema ni kweli alimkopesha Sh 130,000 kwa ajili ya kununulia godoro, lakini alikanusha kudai godoro hilo au fedha. 

Maalim Seif Avitembelea Vyombo vya Habari vya Serikali

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Yussuf Omar Chunda (katikati) akitoa ufafanuzi juu ya shughuli zinazofanywa na Idara hiyo, wakati Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipofanya ziara ya kutembelea Idara hiyo.

Saturday, February 11, 2012

HERE IS BLUE IVY CARTER

TMZ reports:
This is what the heir to a hip-hop fortune looks like ...
Beyonce and Jay Z have finally posted photos of Blue Ivy Carter .. which appear to have been taken at their pimped out suite at Lenox Hill Hospital in NYC.
The Carters posted a note along with the pics which reads, "We welcome you to share in our joy."
Blue Ivy was born on January 7th.
It appears Beyonce color coordinated for the shoot with Blue Ivy ... check out her blue fingernail polish.

Sunday, January 29, 2012

BIBI KIJANA NDANI YA TMK WANAUME FAMILY










Huyu ndio bibi ambae ana rap na kuimba, maajabu yake ameyaonyesha kwenye XXL ya CLOUDS FM leo, stori kamili nitaiweka baadae kidogo hapa hapa millardayo.com na itasikika pia kwenye AMPLIFAYA.





ana umri wa miaka 51, na mpaka sasa hajapata jina la kisanii la kutumia, track yake ya kwanza ameitoa leo kafanya na MH TEMBA
source:millardayo.com